
Siku chache zilizopita msanii Bruno K alimtoa mwimbaji wa zamani wa Bigtym, Oscar kutoka kwenye lindi la umaskini.
Hitmaker huyo wa Omulwa alimchuka msanii huyo na akaanza kumpa support, huku akiongoza kampeni ya kufufua kipaji chake cha muziki ambacho kilikuwa kimefifia.
Sasa baada ya Oscar kupata afueni ameibuka na kumshutumu vikali Bruno K kwa madai ya kutogawa kwa usawa pesa walizopokea kutoka kwa wasamaria wema.
Msanii huyo amehoji ni kwa nini Bruno K mwanzo alikuwa anajifanya anajali sana ilhali alikuwa na ajenda zake za kujinufaisha kupitia jina lake.
Hata hivyo Oscar ametoa changamoto kwa Bruno k kuonyesha namna pesa walizopokea kutoka kwa waganda na makampuni mbalimbali ilivyotumika.