Entertainment

OTILE BROWN AFUNGUKA SABABU ZA KUACHANA NA NABAYET

OTILE BROWN AFUNGUKA SABABU ZA KUACHANA NA NABAYET

Msanii wa muziki nchini, Otile Brown amesema moja ya sababu ya kuachana na mpenzi wake, Nabayet (Nabii) kutokea Ethiopia ni mrembo huyo kutokuwa tayari kuhamia nchini Kenya.

Akizungumza na Presenter Ali, Otile Brown amesema Nabayet alishindwa kuhamia Kenya kwa sababu ya baadhi ya masuala ya kifamilia ambayo yalikuwa muhimu sana katika tamaduni za Waethiopia.

Mahusiano hayo ya muda mrefu hayakufaulu kwa sababu zisizoweza kuepukika kwani wakati mwingine Nabii alikuwa akichukua muda mrefu sana kurejea Kenya.

Otile ambaye amewahi kuwa na mrembo Vera Sidika kipindi cha nyuma, alisema kuwa wote wawili walikubali na kuamua kuachana, na labda ikiwa imepangwa wao kuoana, inaweza kutokea siku zijazo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *