Entertainment

PALLASO AKWEPA KESI YA KUVUNJA MKATABA NA MENEJA IVAN KARMA

PALLASO AKWEPA KESI YA KUVUNJA MKATABA NA MENEJA IVAN KARMA

Msanii Pallaso ameripotiwa kudinda kutii amri ya mahakama baaada ya meneja wake wa zamani Ivan Karma kumfungilia mashtaka kwa madai ya kukiuka mkataba wa miaka mitano wa kufanya kazi pamoja.

Kulingana na wakili wa Ivan Karma, Pallaso amekuwa akikwepa kutia saini stakabadhi muhimu kwa kudai kuwa ameshikika na majukumu yake ya kikazi.

Pallaso anaidaiwa kusaini mkataba unaompa Ivan Karma haki ya kuandaa shows na kutangaza kazi zake za muziki maeneo mbali mbali duniani.

Jukumu la pallaso lilikuwa tu kuimba hadi pale alipoanza kufanya shows zake mwenyewe mara baada ya kutofautia kimawazo na Ivan Karma kutokana na masuala ya fedha.

Mpaka sasa Pallaso ameandaa shows 90 bila uwepo wa Ivan Karma jambo ambalo limemfanya meneja wake huyo wa zamani kumtaka awajibikie shows hizo alizofanya bila idhini yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *