Briefs

Pastor Kanyari Aibua Mjadala kwa Kutoza Waumini Ada ya KSh300 ya Uanachama

Pastor Kanyari Aibua Mjadala kwa Kutoza Waumini Ada ya KSh300 ya Uanachama

Mchungaji mwenye utata Victor Kanyari amezua gumzo mtandaoni baada ya kutangaza kuwa waumini wa kanisa lake watalazimika kujisajili rasmi kwa ada ya KSh 300, ambayo italipwa kila mwezi ili kudumisha uanachama wao.

Kulingana na tangazo hilo, waumini ambao hawatalipa ada hiyo hawatahesabiwa kama wanachama kamili wa kanisa, hali ambayo imezua hisia mseto kutoka kwa umma na wadau wa dini. Wapo wanaoona kuwa hatua hiyo ni aina ya biashara ya kiroho, huku wengine wakihalalisha kwa kusema ni njia ya kusaidia kugharamia huduma za kanisa.

Hii si mara ya kwanza Kanyari kuzua utata. Mchungaji huyo amekuwa akihusishwa mara kwa mara na mbinu tata za uongozi wa kidini, ikiwemo madai ya kutumia miujiza bandia katika ibada zake za awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *