Socialite maarufu nchini Kenya, Amber Ray, ameonyesha wazi kuunga mkono kupitishwa kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uhalifu wa Mtandaoni (Cybercrime Amendment Bill), akisisitiza kuwa uhuru wa kujieleza haupaswi kutumiwa kama kisingizio cha ukatili, uchochezi au kukosa heshima mtandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Amber Ray amesema kuwa anaamini sheria hiyo itasaidia kuweka mipaka kwa watumiaji wa mitandao wanaotumia uhuru wa maoni vibaya kwa kueneza chuki na taarifa za uongo.
Kauli yake imezua mjadala mpana mtandaoni, baadhi ya watumiaji wakimuunga mkono wakisema sheria hiyo itasaidia kudhibiti unyanyasaji na uvunjaji wa heshima, huku wengine wakieleza wasiwasi kwamba inaweza kutumiwa vibaya kukandamiza maoni ya wananchi.
Amber Ray amekuwa miongoni mwa watu mastaa wanaokumbwa mara kwa mara na mashambulizi ya maneno na uvumi mtandaoni, hali ambayo huenda imechangia msimamo wake wa kuunga mkono muswada huo.