
Mwanamuziki nyota kutoka Nigeria, Patoranking, leo ametembelea kambi ya mazoezi ya klabu ya Borussia Dortmund iliyoko Fort Lauderdale, Florida, Marekani.
Kupitia kurasa rasmi za Borussia Dortmund, picha kadhaa zimeonesha msanii huyo akikutana na wachezaji wa timu hiyo, akisalimiana nao na kubadilishana mawazo. Uongozi wa klabu hiyo umeeleza kufurahishwa na ujio wa Patoranking, wakisema ilikuwa heshima kubwa kumpokea kambini. Dortmund kwa sasa inashiriki michuano ya FIFA Club World Cup kama mwakilishi wa bara la Ulaya.
Licha ya mafanikio yake katika muziki wa Afrobeats, Patoranking pia ni mdau mkubwa wa michezo nchini Nigeria. Mchango wake umeonekana wazi kupitia juhudi za kuinua vipaji vya vijana, ikiwemo ujenzi wa uwanja wa soka kwa ajili ya maendeleo ya michezo na jamii kwa ujumla.