
Huenda penzi la mwanamuziki na C.E.O.wa KondeGang Harmonize na mpenzi wake mzungu raia wa Australia Briana limevunjika.
Kulingana na mfululizo wa post zake kupitia insta story yake kwenye mtandao wa instagram harmonize amesema kuwa haamini kama yupo singo tena.
Haikuishia hapo ameenda mbali na kuandika ujumbe ambao unahisiwakumlenga moja kwa moja mchumba wake Briana kwa kusema tuonane nikifikisha umri wa miaka 35 labda nina umri wa miaka.
Hata hivyo Harmonize hajatoa maelezo zaidi kuhusu kiini cha uhusiano wake na Briana kuvunjika ila walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji kuwa huenda msanii huyo wa Bongofleva anatengeza mazingira ya kumzungumziwa Afrika Mahariki kabla ya ujio wa ngoma yake mpya
Ikumbukwe kuwa penzi la Harmonize na Briana lilianza rasmi mwishoni mwa mwaka jana miezi kadhaa baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Fridah Kajala.
Mbali na hayo mwanamuziki huyo ametangaza kuachia wimbo wake mpya siku ya kesho unaitwa ‘Mwaka Wangu’