Entertainment

PENZI LA JULIANA KANYAMOZI LAMKOSESHA USINGIZI NAMELESS

PENZI LA JULIANA KANYAMOZI LAMKOSESHA USINGIZI NAMELESS

Msanii mkongwe nchini Nameless ameshindwa kuficha mapenzi yake kwa msanii wa kike nchini Uganda Juliana Kanyamozi.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Nameless amesema asingekuwa ameoa  angemchumbia mwanamuziki huyo kwa kuwa ni mrembo, ana kipaji cha kipekee lakini pia ni mchapa kazi.

Hitmaker huyo wa ngoma “Deep” ameenda mbali zaidi na kusema kwamba wamekuwa marafiki kwa kipindi kirefu kwenye shughuli zao za kimuziki.

Hata hivyo watumiaji kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kushangaza na kauli ya rapa huyo wengi wakihoji huenda  Nameless ana kazi ya pamoja na Juliana Kanyamozi hivyo anatengeneza mazingira ya kuzungumuziwa kabla ya ujio wa ngoma yao mpya.

Nameless amesema hayo alipokuwa nchini uganda ambako alikuwa ameenda kwa ajili ya kutumbuiza kwenye onesho la Comedy Store.

Utakumbuka Nameless alifunga ndoa na msanii mwenzake Wahu mwaka wa 2005 na wabarikiwa na watoto wawili ambao ni Tumiso na Nyakio.

Ndoa ya wanamuziki hao imedumu muda mrefu kinyume na matarajio ya wengi kutokana na jinsi watu maarufu wamekuwa wakiacha ndoa zao ulimwenguni kote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *