
Mrembo maarufu mtandaoni nchini Pritty Vishy amethibitisha kutokuwa na maelewano mazuri na mchumba wake msanii Madini Classic.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Mrembo huyo amesema kwa muda sasa hawajakuwa pamoja na Madini Classic kutokana na ugomvi ulioibuka kati yao juzi kati.
Vishy amedai kwamba kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kutatua tofauti zao huku ukisisitiza kuwa ikitokea hawatapa mwarubaini wa ugomvi wao huenda wakavunja mahusiano yao rasmi.
Kauli ya Pritty Vishy imepingwa vikali na Madini Classic ambaye amedai kuwa hawana tofauti zozote na mrembo huyo huku akikazia kuwa penzi lao lipo imara licha ya kutoonekana wakiwa pamoja katika siku za hivi karibuni.