
Msanii nyota nchini Jovial amekiri kupata mashabiki wengi wanaofuatilia kazi zake tangu atangaze kuingia kwenye mahusiano na Willy Paul.
Kupitia insta story mrembo huyo ameshindwa kuficha furaha yake kwa kusema kwa kipindi chote cha maisha ya muziki hajawahi pata idadi kubwa ya watu wanaotazama nyimbo zake pamoja na kutembelea mitandao yake ya kijamii licha ya kushirikiana na wasanii mbali mbali kwenye suala la kuachia nyimbo kali.
Katika hatua nyingine Mrembo huyo amesema ameshangazwa namna watu wanavyomshambulia Β na Willy Paul kwa kujihusisha na kiki mtandaoni ilhali hawaungi mkono kazi za wasanii wachanga wanaotoa muziki mzuri bila kutengeneza matukio.
Hata hivyo amemaliza kwa kuachia Wakenya swali kama wanaunga mkono muziki mzuri au umbea ambapo mashabiki wengi wameonekana kusisitiza umuhimu wa wasanii kutoa muziki mzuri sambamba na kutengeneza matukio yatakayowafanya wazungumziwe mtandaoni kama njia ya kujitangaza kimuziki.