Gossip

Pipi Jojo Akanusha Kubebeshwa Ujauzito na Baba Yake wa Kumlea, Chief Godlove

Pipi Jojo Akanusha Kubebeshwa Ujauzito na Baba Yake wa Kumlea, Chief Godlove

Msanii chipukizi wa Bongofleva, Pipi Jojo, amekanusha vikali madai yanayosambaa mitandaoni yanayodai kuwa amebebeshwa ujauzito na baba yake wa kumlea, Bilionea Chief Godlove.

Kupitia video aliyochapisha mitandaoni, Pipi Jojo amekanusha vikali madai hayo, akisisitiza kuwa hana ujauzito wowote. Ameeleza kuwa uhusiano wake na Chief Godlove ni wa kifamilia na kikazi, akimtaja kama baba wa kumlea, mfadhili na mwekezaji katika safari yake ya muziki. Ameongeza kuwa amekuwa akimsaidia kwa kiwango kikubwa kufanikisha ndoto zake katika tasnia ya muziki.

Msanii huyo amebainisha kuwa uvumi huo umeanza kumuathiri baba yake kiafya kutokana na msongo wa mawazo, hali iliyomlazimu kutoa wito kwa jamii kuacha kueneza taarifa za uongo.

Hata hivyo, ameomba heshima itunzwe ili kuepusha madhara zaidi, hasa ikizingatiwa mchango mkubwa anaoutoa Chief Godlove katika kusaidia yatima na jamii kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *