Entertainment

Pritty Vishy Afunguka Sababu za Kuogopa Ndoa

Pritty Vishy Afunguka Sababu za Kuogopa Ndoa

Socialite na mratibu wa maudhui mtandaoni, Pritty Vish, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu sababu zinazomfanya awe na hofu kubwa ya kuingia katika ndoa, akieleza kuwa historia ya familia yake imempa mtazamo tofauti kuhusu maisha ya kifamilia.

Kupitia mitandao yake kijamii, Pritty amesema kuwa amekua katika mazingira yaliyomjenga kuwa mwangalifu, baada ya kuona jinsi mama yake alivyojitoa bila kupokea msaada wowote kutoka kwa baba yake, ambaye anadaiwa kutokuwa mwaminifu na kushindwa kutoa mahitaji ya msingi kwa familia.

Kwa mujibu wa Pritty, mama yake alilazimika kumlea peke yake kutokana na tabia za baba yake ambazo zilimsababisha kupata maumivu makubwa ya kihisia na kiuchumi. Ameeleza kuwa tukio hilo limemuathiri na kumfanya kuwa na wasiwasi kuhusu kuingia katika ndoa ambayo inaweza kumrudisha kwenye majeraha aliyoyaona akiwa mdogo.

Pritty anasema kuwa licha ya kuwa na mtazamo huo, bado anaamini katika upendo, lakini atachukua muda wake kuhakikisha anamjua vema mtu atakayechagua kuwa naye maishani. Ameongeza kuwa matarajio yake ya ndoa ni kuwa na mwenzi anayewajibika, mkweli na mwenye roho ya kujali familia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *