Entertainment

Pritty Vishy akata tamaa kwenye penzi la Daddy Owen.

Pritty Vishy akata tamaa kwenye penzi la Daddy Owen.

Mrembo asiyeishiwa na matukio kila leo Pritty Vishy amekata tamaa kwenye penzi la Daddy Owen ikiwa ni siku chache zimepita toka mwimbaji huyo wa injili amkatae hadharani.

Mrembo huyo ambaye kwa wakati mmoja aliwahi kuwa penzini na msanii Stivo Simple Boy amemtaja Daddy Owen kama dikteta asiyekuwa na msimamo mara baada ya kusisitiza kuwa mwanamke wa ndoto yake lazima ajue kuzungumza lugha ya Kiingereza kwa ufasaha lakini pia asiwe mtumiaji wa mtandao wa Tiktok.

Hata hivyo amemalizia kwa kumshauri hitmaker huyo wa Vanity kutimukia nchini Uganda iwapo anataka kufanikisha mchakato wa kupata mke wa kuingia naye kwenye ndoa kwani wasichana wa Kenya hawana ufasaha wa lugha ya Kiingereza.

“Nilikua namtaka lakini sasa penye inaelekea ni kama itabidi avuke Uganda. He’s like a dictator. Sijui hataki dem ako TikTok, anataka dem anajua Kizungu mingi. Ikifika mahali ya TikTok na Kizungu mingi avuke tu Uganda. Hapa Kenya tuko TikTok na tunaongea Kizungu ya kilami. Ugandans ndio wako bushy,” Alisema.

Utakumbuka mara baada ya Daddy Owen kutangaza kuwa anatafuta mke wa kuingia naye kwenye ndoa mapema wiki iliyopita, amepokea zaidi ya maombi 10,000 kutoka kwa wanadada tofauti ambao wametia nia ya kumtaka kimahusiano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *