Mtayarishaji na mwongozaji wa muziki nchini Kenya, JBlessing, ametoa albamu mpya yenye nyimbo 14 iliyopewa jina “RAILA”, kama heshima kwa hayati Raila Amolo Odinga.
Albamu hiyo, ambayo imetolewa rasmi jana, inalenga kumuenzi kiongozi huyo wa kisiasa ambaye maisha na urithi wake umeacha alama kubwa katika historia ya taifa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, JBlessing ameeleza kuwa historia ya Raila inaendelea kupitia muziki, akihimiza mashabiki kutazama na kusikiliza nyimbo zote 14 kutoka kwa bendi ya Maestro kwenye YouTube na majukwaa yote ya muziki mtandaoni.
Albamu ya “RAILA” inahusisha ushirikiano na bendi ya Maestro, na imeandaliwa kwa mchanganyiko wa mitindo ya muziki tofauti ikiwemo soul, afro-fusion na muziki wa kisasa wa Kiafrika.