
Prodyuza wa muziki kutoka nchini Uganda Artin Pro amejitenga na madai ya kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa wasanii wa kike ili aweze kuwasaidia kutanua wigo wao kimuziki.
Artin amesema anaheshimu kazi yake ya kutayarisha muziki, hivyo hawezi kuwa na tamaa ya kuwataka kimapenzi na wasanii wa kike kwa kuwa ni wateja wake wanaompa kazi inayomuingizia kipato.
“Sijawahi na siwezi kwa sababu naheshimu kazi yangu. Siwezi kutoka kimapenzi na wasanii wakike, hao ndio wateja wangu wakubwa,” alisema Artin.
Artin Pro ni moja kati ya maprodyuza walioacha alama kwenye muziki wa Uganda kwa kipindi cha mwongo mmoja kutokana nyimbo kali ambazo amekuwa akizitayarisha.
Ikumbukwe prodyuza mwenzake Daddy Andre aliwahi kutuhumiwa kuwanyanyasa kingono wasanii wa kike katika harakati za kuwasaidia kisanaa.