Entertainment

Rapa 50 Cent adokeza ujio wa ngoma mpya na mtayarishaji nguli Dr. Dre

Rapa 50 Cent adokeza ujio wa ngoma mpya na mtayarishaji nguli Dr. Dre

Baada ya hivi karibuni kudokeza kuwa anafanyia kazi ujio mpya wa kazi zake za muziki kwa mwaka 2023, Rapa 50 Cent ametusanua kuhusu ujio wa ngoma mpya na mtayarishaji nguli Dr. Dre.

Kwenye mahojiano na mtangazaji Big Boy, 50 Cent amekaririwa hapo akisema tutarajie ushirikiano wao tena kwa mara nyingine kwani baada ya kutangaza kurudi kwenye muziki alipokea ujumbe mfupi kutoka kwa Eminem ambao ulisema, Dr. Dre ana midundo kwa ajili yake.

Ujio wa 50 Cent kwenye dunia ya muziki miaka 20 iliyopita ilifanikishwa na kazi kubwa ya Mtayarishaji Dr. Dre ambaye alipika midundo mizito iliyoweza kunata vyema kwenye mistari ya Rapa huyo ambaye alishikwa mkono na Eminem.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *