Entertainment

Rapa Gravity Omutujju akiri kumchukia Spice Diana na meneja wake Rodger Lubega

Rapa Gravity Omutujju akiri kumchukia Spice Diana na meneja wake Rodger Lubega

Rapa Gravity Omutujju na Spice Diana walikuwa marafiki wakubwa sana kwa muda mrefu hadi alipokosana kutokana na sababu ambazo hawakuweka wazi.

Wakati wa mahojiano hivi karibuni, Gravity amefichua kwamba anachukia uongozi wa Spice Diana kiasi kwamba hakutaka kusikia chochote kuhusu tamasha la mrembo huyo lililokamilika hivi karibuni.

“Sikusikia kuhusu tamasha lake. Sikujua chochote kuhusu yeye pamoja na meneja wake. Siwapendi,” alisema kwenye mahojiano na Galaxy TV.

Rapa huyo ameendelea kumlaani meneja wa Spice Diana, Rodger Lubega kwa madai ya kuwa mtu mbaya ambaye amekuwa akihujumu shughuli za watu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *