Entertainment

Rapa Toxic Lyrikali Adharau Diss Track ya Wakuu Music

Rapa Toxic Lyrikali Adharau Diss Track ya Wakuu Music

Rapa anayeongoza katika chati za muziki nchini Kenya, Toxic Lyrikali, amepuuza kwa dharau ‘diss track’ iliyomlenga iliyotolewa na kundi la Wakuu Music, akieleza kuwa hana muda wa kujibu migogoro inayoendeshwa na wivu na chuki kutokana na mafanikio yake.

Kupitia Instagram Live, Toxic Lyrikali amesema wazi kuwa hawezi kamwe kujibu diss track kutoka kwa wasanii ambao “hata hawana blue tick,” akimaanisha hawathibitishwi au kutambulika rasmi kwenye mitandao ya kijamii.

Akieleza sababu ya kutojibu kwa wimbo, Lyrikali amesema hatua yake haitokani na kushindwa, bali ni kutokana na ukweli kwamba ‘diss track’ ya Wakuu Music haikidhi viwango vya rap.

Rapa huyo ametoa wito kwa wasanii wote wanaotaka kumkosoa kwa nyimbo kutafuta mashairi yenye uzito na pointi za maana badala ya kujidhalilisha na diss tracks ambazo hazina uzito.

Hata hivyo amewashukuru mashabiki wake kwa sapoti kubwa anayoipata, akiwahakikishia kuwa kutojibu kwake hakuleti shaka yoyote kuhusu uwezo wake kwani kazi yake ndiyo jibu lake kuu.

Wakuu Music walikuwa wameachia diss track hiyo maalum wakimtaka Toxic Lyrikali ajibu kwa mashairi, lakini amekataa kabisa kuingia kwenye vita ya maneno akisema hajishughulishi na wasanii wanaotafuta kiki kupitia jina lake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *