Entertainment

Rapa Wakazi Amkingia Kifua Master Jay Dhidi ya Kubezwa na Wasanii

Rapa Wakazi Amkingia Kifua Master Jay Dhidi ya Kubezwa na Wasanii

Rapa Wakazi, ameonyesha kutopendezwa na namna ambavyo mtayarishaji nguli Master Jay amekuwa akibeuliwa na baadhi ya wasanii na producers wa kizazi cha sasa.

Kupitia ujumbe alioweka kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Wakazi ameeleza kusikitishwa na hali hiyo, akibainisha kuwa mchango mkubwa wa Master Jay katika tasnia ya muziki wa Tanzania haupaswi kusahaulika wala kubezwa.

Rapa huyo amesema huenda ukaribu wa Master Jay na wasanii wachanga umewafanya baadhi yao kumpuuza, huku wengine wakisahau historia na mchango wake katika sekta ya burudani.

Wakazi pia amesisitiza kuwa tatizo kubwa ni ukosefu wa kumbukumbu na heshima kwa walioweka msingi wa muziki wa Bongofleva, akihimiza wasanii chipukizi na hata wakongwe kutambua mchango wa waliotangulia.

Kauli ya Wakazi imeibuka baada ya msanii mkongwe Juma Nature kunukuliwa katika moja ya mahojiano akidai hajawahi kumkubali Master Jay kama producer. Nature alieleza kuwa kipindi hicho Master Jay alitamani kuwa kama P Funk Majani, hali iliyomfanya baba yake mzazi kumnunulia vyombo vya muziki na si kwa ubunifu au kipaji chake binafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *