
Wanamuziki nyota wanaoiwakilisha vyema Afrika Mashariki, wasanii Rayvanny na Otile Brown wameingia studio na wameonekana kwenye upishi wa kazi mpya.
Wawili hao wanatajwa kuingia studio usiku wa kuamkia leo katika studio za Next Level Music zilizopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam, zilizo chini ya msanii Rayvanny.
Hata hivyo, bado haijafamika kuwa hii itakuwa ni kazi ya nani, tarajia kuipata kazi hiyo kutoka kwa wawili hao siku za usoni.