Entertainment

Recho Ray akanusha kughushi noti ya shillingi elfu 50 Uganda

Recho Ray akanusha kughushi noti ya shillingi elfu 50 Uganda

Msanii Recho Ray amejitenga na picha inayosambaa mtandaoni ikimuonesha akiwa kwenye noti ya shilling elfu 50 ya Uganda ambapo alikuwa ameanika wazi maungo yake ya mwili.

Recho Ray anasema picha hizo zilichapishwa na watu waliodukua akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Facebook.

“Hey, guys my account is restored now. It was hacked,” Aliandika Instagram.

Lakini mashabiki zake wanahoji kuwa anajaribu kukwepa msala wa kufunguliwa kesi kwa madai ya kughushi nyaraka za serikali.

Ikumbuke ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kuchapisha noti au sarafu yoyote ya Benki Kuu nchini Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *