
Mwanamuziki asiyeishiwa na matukio kila leo Ringtone Apoko amefunguka tusiyoyajua kuhusu ukimya wa Bahati kwa kusema kwamba amekuwa chimbo akiandaa EP yake mpya.
Kulingana na Ringtone hatua ya Bahati kufuta kila kitu kwenye ukurasa wake wa Instagram ilikuwa ni njia ya kutengeneza mazingira ya ujio wa EP hiyo ambayo ina jumla ya nyimbo 6.
Katika hatua nyingine Ringtone amewataka mashabiki kumweka Bahati kwa maombi kwa sababu mkali huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amekuwa na msongo wa mawazo tangu ashindwe kwenye kinyanganyiro cha ubunge Mathare.
Bahati amekuwa kimya baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9 kukamilika nchini Kenya, jambo ambalo liliwaacha mashabiki zake na maswali mengi kiasi cha kutaka kufahamu ni nini hasa kimemsibu msanii huyo.