
Msanii asiyeishiwa na matukio kila leo Ringtone Apoko amemtolea uvivu Eric Omondi baada ya mchekeshaji huyo kutamba na mbwa wake kwenye uzinduzi wa onesho la Laugh & Jazz mwishoni mwa juma lillopita.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ringtone amedai kuwa Omondi alimuomba mbwa hao kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwenye vyombo vya habari nchini.
Hitmaker huyo wa “Ombi Langu” amesema licha ya kumsaidia Omondi kufanikisha jambo lake amekerwa na kitendo cha mchekeshaji huyo kumregeshea mbwa wake wakiwa wachafu na wachovu.
Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wamemuashia moto Ringtone kwa madai ya kutafuta kiki kupitia jina la Omondi.