Gossip

Ruth K Aomba Msamaha kwa Baba Yake Baada ya Video ya Faragha Kusambazwa

Ruth K Aomba Msamaha kwa Baba Yake Baada ya Video ya Faragha Kusambazwa

Mrembo na mshawishi maarufu mitandaoni, Ruth K, ameomba msamaha wa dhati kwa baba yake na familia nzima baada ya video ya faragha inayodaiwa kurekodiwa na aliyekuwa mpenzi wake Mulamwah kusambazwa bila idhini yake.

Kupitia mitandao ya kijamii, Ruth alieleza kuwa amevunjika moyo na kuumizwa na tukio hilo, akielezea majuto yake kwa kile alichokitaja kuwa ni aibu kubwa kwa familia. Alisisitiza kuwa hajakusudia kuwakosea heshima wazazi wake na kwamba amejifunza somo muhimu kuhusu faragha, uaminifu, na mipaka katika mahusiano.

“Nimejifunza kuwa video ya faragha imetumwa kwako na aliyekuwa mpenzi wangu. Nimevunjika moyo. Nipo magotini nikiomba msamaha kwa kukuangusha wewe na familia yetu. Tafadhali nisamehe.” Aliandika Instagram.

Ruth K amesema ataendelea kuelimisha na kupaza sauti dhidi ya ukatili wa kimtandao, na kutumia uzoefu wake kama somo kwa wengine, hususan vijana na wanawake wanaopitia hali kama hiyo.

Video hiyo, ambayo haikufafanuliwa kwa kina, imezua mijadala mikali mitandaoni kuhusu usalama wa taarifa binafsi na matumizi mabaya ya maudhui ya faragha, hususan baada ya kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi.