
Sam West amethibitisha kuvunjika kwa mahusiano yake na mwimbaji Vivian baada ya kudumu kwenye ndoa kwa muda wa takriban miaka sita.
Kupitia ujumbe wa mafumbo aliouchapisha kwenye mtandao wa Instagram Sam West aamesema ameamua kuachana na mwimbaji huyo kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wake kwani angendelea kubaki kwenye mahusiano hayo huenda angepoteza maisha yake kutokana na msongo wa mawazo.
Kauli ya Sam West inakuja baada ya Vivian kuweka wazi kuwa anapitia kipindi kigumu katika maisha kufuatia mume wake kumkimbia ambapo alienda mbali zaidi na kuwataka mashabiki wamweke kwa maombi kutokana na jini mkata kamba kuingilia mahusiano yake.
Hata hivyo mashabiki walitilia shaka taarifa za mrembo huyo kuachana na mume wake Sam West wengi wakihoji kuwa huenda anatafuta njia ya kuteka hisia zao kwa ajili ya ujio wa ngoma yake mpya.
Utakumbuka wawili hao wamekuwa pamoja tangu mwaka wa 2016 baada ya Sam West kumvisha pete ya uchumba Vivian mubashara kwenye kipindi cha runinga ambapo mwaka wa 2018 walihalalisha mahusiano yao kwa njia ya harusi ya kitamaduni.