
Mwanamuziki na mwigizaji maarufu, Selena Gomez, ameonekana kuonyesha mshikamano wa kimya lakini wa dhati kwa Hailey Bieber, mke wa zamani wa mpenzi wake, Justin Bieber, kufuatia kauli ya kuumiza aliyotoa Justin kuhusu jarida la Vogue.
Hili limetokea baada ya Justin Bieber kufichua kuwa aliwahi kumwambia Hailey kuwa hatawahi pata nafasi ya kuwa kwenye jalada la jarida la Vogue, kauli ambayo wengi waliiona kama ya kubeza ndoto na uwezo wa Hailey katika tasnia ya mitindo
Wakati gumzo hilo likiendelea kuchukua nafasi mtandaoni, Selena Gomez alionekana kuonyesha ishara ya kuunga mkono upande wa Hailey kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kwa ku-like chapisho moja kwenye mitandao ya kijamii lililompongeza Hailey kwa ustahimilivu wake. Kitendo hicho kimefasiriwa na mashabiki wengi kama njia ya kuonyesha huruma na mshikamano, licha ya historia yao ya mapenzi na Justin.
Mashabiki wameisifu Selena kwa ukomavu na utu alioonyesha, wakisema kwamba hatua yake ni ya kipekee na inathibitisha kuwa wanawake wanaweza kusimama pamoja hata katika hali tata za kihisia.
Hadi sasa, Hailey Bieber hajatoa kauli rasmi kuhusu tukio hilo, lakini ishara ya uungwaji mkono kutoka kwa Selena imeonekana kama faraja kwa wengi walioguswa na kauli ya Justin.