Entertainment

Sheebah hakunilipa chochote kutumbuiza kwenye shoo zake – Chozen Blood

Sheebah hakunilipa chochote kutumbuiza kwenye shoo zake – Chozen Blood

Msanii kutoka nchini Uganda Chozen Blood amefunguka madai ya kulipwa na msanii Sheebah Karungi kwenye tamasha lake la siku mbili lilofanyika kwenye hoteli ya Serena na Freedom City mwishoni mwa juma lilopita.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Chozen Blood amesema hakupokea hata senti moja kutoka kwa Sheebah kutumbuiza kwenye matamasha yake mawili ambayo yalipokea upendo mkubwa kutoka kwa mashabiki.

“Nilitumbuiza Freedom City na siku mbili  Serena. Hakunilipa chochote,” alisema wakati wa mahojiano yake.

Utakumbuka hivi karibuni Mwanamuziki Crysto Panda aliwataka wasanii kutumbuiza bila malipo kwenye shoo za wasanii wenzao huku Rickman Manrick akiwataka wasanii kudai malipo kila mara wanapoalikwa kwenye matamasha za muziki kabla ya kupanda jukwaani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *