Influencer wa Kenya, Shorn Arwa, amejizawadia gari jipya aina ya Toyota Harrier lenye vifaa kamili kwenye siku yake ya kuzaliwa, hatua iliyozua pongezi na gumzo mitandaoni.
Kupitia chapisho lake la kusherehekea birthday yake, Shorn Arwa ameonyesha shukrani kubwa kwa Mungu na kujivunia hatua aliyofikia, akieleza kuwa mambo aliyokuwa akiyaomba hapo awali sasa yamekuwa sehemu ya maisha yake ya kila siku. Katika ujumbe wake, amesema kuwa kujinunulia gari hilo ni ushahidi wa kazi, nidhamu na kujitokeza kila siku kwa ajili ya ndoto zake.
Mrembo huyo, amefafanua kuwa Toyota Harrier hiyo mpya imenunuliwa kwa jina lake halali la kiserikali, jambo alilosisitiza kwa furaha akieleza kuwa ni SUV yenye vifaa vyote vya kisasa.
Shorn Arwa pia amejipongeza kwa juhudi na uthubutu wa kuendelea kusukuma mbele licha ya changamoto, akihitimisha ujumbe wake kwa kujitakia heri ya siku ya kuzaliwa kwa maneno yaliyojaa upendo na matumaini makubwa ya mafanikio zaidi.