Entertainment

Snoop Dogg Ahoji Maudhui ya Filamu ya Watoto Baada ya Kutazama Lightyear

Snoop Dogg Ahoji Maudhui ya Filamu ya Watoto Baada ya Kutazama Lightyear

Rapa mkongwe wa Marekani, Snoop Dogg, amesema kuwa hana tena amani ya kwenda kuangalia filamu kwenye sinema baada ya kushuhudia mjukuu wake akimuuliza maswali magumu alipowaona wahusika wa mapenzi ya jinsia moja wakionyeshwa kwenye filamu ya Lightyear.

Kwa mujibu wa Snoop, alishtushwa na mjukuu wake kuuliza maswali baada ya kuona wapenzi wa kike (lesbian couple) ndani ya filamu hiyo ya watoto. Tukio hilo, amesema, lilimfanya ahisi wasiwasi kuhusu maudhui yanayoonyeshwa kwa watoto kupitia filamu kubwa za kimataifa.

Kauli yake imezua mjadala mkubwa mtandaoni, baadhi ya watu wakieleza kuwa wasanii na wazazi wana haki ya kuamua maudhui ya watoto wao, huku wengine wakimkosoa kwa mtazamo wake wakidai anapinga usawa wa jamii ya LGBTQ+.

Filamu ya Lightyear, ambayo ni tawi la hadithi maarufu ya Toy Story, ilizua gumzo kubwa tangu ilipoachiliwa mwaka 2022, hasa kwa sababu ya kuonyesha uhusiano wa ndoa wa jinsia moja kwa mara ya kwanza kwenye sinema ya Disney-Pixar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *