Gossip

Socialite Kate Thuku Asema Wanaume wa Kisasa Hawana Mapenzi ya Kweli

Socialite Kate Thuku Asema Wanaume wa Kisasa Hawana Mapenzi ya Kweli

Socialite chipukizi Kate Thuku ameweka wazi sababu zinazomfanya kwa sasa asiwe kwenye mahusiano ya kimapenzi, akidai kuwa wanaume wengi wa kisasa hawana romance.

Akiwa mgeni kwenye podcast ya Prezident Law, Kate alisema anatilia maanani upendo, hisia na kujitolea katika uhusiano. Hata hivyo, kwa mtazamo wake, wanaume wa kisasa wamepoteza ule msisimko na ugunduzi wa kimapenzi unaofanya mahusiano yawe ya kipekee.

Kate amefichua pia hapendezwi na wanaume wa mashinani kwa sababu, kwa mtazamo wake, mara nyingi huja na masharti makali yanayomnyima uhuru wake. Badala yake, anatamani mwanaume wa kisasa anayeweza kumfanya ajisikie malkia kupitia vitendo vidogo vya kimapenzi kama kumnunulia maua au hata kumwandikia barua za mapenzi.

Kwa sasa, Kate anasisitiza kuwa hana haraka ya kuingia kwenye uhusiano iwapo matarajio yake ya kimapenzi hayatatimizwa, akisema anajipa kipaumbele kujitengenezea furaha na kuendeleza maisha yake binafsi.

Kauli yake imezua mazungumzo makubwa mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakimpongeza kwa kuweka wazi vigezo vyake, huku wengine wakimkosoa wakisema anatafuta mapenzi ya hadithi za vitabuni ambazo si rahisi kupatikana katika maisha ya kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *