Entertainment

SOSUUN NA VIVIAN WASHAMBULIWA MTANDAONI KWA KUTUMIA KIKI KUTANGAZA NGOMA YAO MPYA

SOSUUN NA VIVIAN WASHAMBULIWA MTANDAONI KWA KUTUMIA KIKI KUTANGAZA NGOMA YAO MPYA

Mashabiki wa muziki nchini wamewatolea uvivu wasanii Vivian pamoja na Sosuun baada wasanii hao kuonekana kutumia kiki kutangaza kazi yao mpya ambayo itaingia sokoni hivi karibuni.

Kupitia mitandao yao ya kijamii wawataka Vivian na Sosuun waache suala la kuendekeza kiki kwenye muziki wao na badala yake watoe muziki mzuri ambao utajiuza wenyewe.

Aidha wameenda mbali zaidi na kusema kwamba wasanii hao hawana ubunifu kwenye masuala ya kutengeneza matukio yatakayowafanya wazungumzie mtandaoni kwani kiki waliyotengeneza haina mashiko yeyote ya kuteka hisia za watu.

Kauli hiyo ya wakenya mara baada ya Sosuun kurekodi video akimvamia Vivian akiwa kwenye studio za main switch na kutaka kumshushia kichapo kwa hatua ya kumvunjia heshima mapema wiki aliposema kuwa familia yake ndio imemfanya apotea kwenye game ya muziki nchini licha ya kuwa kipaji.

Utakumbuka kwa sasa Vivian pamoja na Sosuun  wameachia ngoma yao mpya inayokwenda kwa jina la “Chachisha.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *