LifeStyle

Spice Diana Adai Hutumia Milioni 2 za Uganda kwa Siku

Spice Diana Adai Hutumia Milioni 2 za Uganda kwa Siku

Msanii nyota kutoka Uganda, Spice Diana, amefunguka kuhusu kiwango cha pesa anachotumia kwenye mahitaji yake kila siku.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini humo, Spice Diana amesema kuwa hutumia takribani shilingi milioni 2 za Uganda kwa siku, hasa anapokuwa na shoo.

Amesema hata anapokuwa nyumbani bila kufanya maonesho wala kulipa bili kubwa, bado matumizi yake hufikia karibu milioni 1.5 kwa siku.

Kwa mujibu wa mrembo huyo, matumizi hayo yanajumuisha kujitunza binafsi, gharama za usafiri, chakula, maandalizi ya kazi (logistics) pamoja na mahitaji ya jumla ya maisha.

Hata hivyo, Spice Diana anaamini kuwa mafanikio yana gharama, na kwa msanii wa kiwango chake, kuwekeza kwenye mwonekano na uendeshaji wa kazi ni sehemu ya safari ya mafanikio.

Kauli yake imeibua mjadala mpana mitandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wanamsifia kwa uwazi na kujituma kuwekeza kwenye chapa (brand) yake, huku wengine wakiona kiwango hicho cha matumizi ni kikubwa kupita kiasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *