Msanii nyota wa muziki kutoka Uganda, Spice Diana, ameonesha mshangao mkubwa baada ya kushuhudia ongezeko kubwa la wafuasi wake katika mitandao mbalimbali ya kijamii tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2026.
Kupitia Instastory yake, Spice Diana amesema awali alidhani kuwa umaarufu mkubwa mtandaoni huja zaidi na drama, lakini kwa sasa yupo katika kipindi cha amani na bado mafanikio yanaongezeka.
Msanii huyo amefichua kuwa Snapchat views zake zimekuwa za kushangaza, huku TikTok akifikisha zaidi ya wafuasi milioni 2.3. Aidha, ndani ya siku 30 zilizopita pekee, akaunti yake ya Instagram imekusanya zaidi ya views milioni 4.
Ingawa amekiri kuwa idadi hizo zimepungua kidogo katika siku chache zilizopita, amesema bado hali ni nzuri. Sambamba na mafanikio hayo, Spice Diana pia ametangaza kuwa dili mpya ya endorsement iko njiani, ishara kuwa ushawishi wake wa kidijitali unaendelea kuimarika.
Kauli yake imekuja mara baada ya kufichua mwaka jana kuwa hatofanya tamasha lolote la muziki mwaka huu, akieleza kuwa ameamua kuelekeza nguvu zake katika kuwekeza zaidi kwenye majukwaa ya kidijitali.