
Nyota wa muziki kutoka Nigeria Wizkid anaendelea kugonga vichwa vya habari kwa upande wa idadi ya watu wanaofutilia mziki wake kwenye digital platforms mbali mbali za kustream muziki duniani.
Wizkid amefanikiwa kufikisha jumla ya STREAMS Milioni 100 kwenye App namba moja ya kusikiliza na kupakua muziki mtandaoni ya Boomplay Music, Hivyo amejiunga rasmi na Golden Club baada ya kupata idadi hiyo ya streams.
Lakini pia anaungana na wakali wengine kutoka Nigeria waliofikisha idadi hiyo ya streams kupitia Boomplay ambao ni Davido, Omah Lay na Fire Boy.
Utakumbuka wasanii Joeboy na Burna Boy tayari wana streams zaidi ya Milioni 200.