
Msanii Stevo Simple Boy ameachia wimbo uitwao ‘ Haya basi ‘ ambapo ameeleza manyanyaso aliyoyapitia kwenye shoo ambayo alishindwa kutumbuiza huko Mombasa.
Kwenye wimbo huo, Stevo amemtolea uvivu mchekeshaji Eric Omondi kwa kupendekeza autimue uongozi wake wa Men In Business.
” Naskia walisema nifute manager kumbe hao ndio mateja wanajifanya huku nyuma wananipenda na kumbe hao hao ndio wananisema.”
Stevo Simple Boy ameeleza namna ambavyo Eric Omondi alikuwa anamshinikiza kutoa burudani kwa mashabiki zake bila malipo kwenye tamasha la Sofire fiesta
” Ati Simple kuja show nitakulips baada ya show nakula matumbo, wakaleta zogo.”
Msanii huyo amedai kuwa Eric Omondi alitumia sakata lake la kutolipwa na waandaaji wa Sofire fiesta kutafuta kiki ili azungumziwe kwenye mtandaoni ya kijamii.
” Naskia kiki, naskia simple kwenye basi, haya basi, napigwa picha Hadi nikikunywa Maji, naskia vitu mingi Yule Rais ni wa nini?”
Utakumbuka Mwishoni mwa mwezi Desemba 2022, Stivo Simple Boy alifichua kwamba alishindwa kutumbuiza huko Mombasa baada ya waandaji wa sofire fiesta kukataa kumlipa pesa zake kabla ya kutoa burudani kwa mashabiki zake.
Kitendo hicho kilimkasirisha Eric Omondi ambaye alikashifu uongozi wa Stevo akiulaumu kwa masaibu yaliyompata mwanamuziki huyo. Omondi alidai kuwa mameneja hao walizembea kwenye kazi yao kwa kumpeleka Stevo Mombasa bila mpangilio wowote ambapo alienda mbali na kupendekeza wajiuzulu.