LifeStyle

Stevo Simple Boy Anawishwa Mikono na Pombe ya KSh 100,000

Stevo Simple Boy Anawishwa Mikono na Pombe ya KSh 100,000

Msanii wa muziki wa Kenya, Stevo Simple Boy, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kuposti video ikimuonesha akioshwa mikono na bilionea Chief Godlove kwa kutumia pombe ghali zaidi aina ya Clase Azul kwenye moja ya nightclub Jijini Nairobi.

Katika video hiyo iliyosambaa kwa kasi mtandaoni, Stevo anaonekana akifurahia tukio hilo huku akionekana mwenye bashasha. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Stevo Simple Boy ameeleza kwamba, kwa mtazamo wake, matumizi ya pombe au mihadarati hayafai kwa ulevi au matumizi mabaya, bali yanaweza kuwa mfano wa usafi na nidhamu katika maisha.

Clase Azul ni moja ya pombe za kifahari duniani, inayotengenezwa nchini Mexico. Nchini Kenya, chupa ya 700 ml ya Clase Azul Plata huuzwa kati ya KSh 24,000 hadi KSh 40,000, huku toleo la Reposado likigharimu kati ya KSh 44,000 na KSh 66,000. Toleo la kifahari zaidi, Clase Azul Gold, linaweza kufikia hadi KSh 159,000 kwa chupa moja, kulingana na maduka ya pombe ya kifahari nchini
humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *