
Msanii wa Men In Business, Stevo The Simple Boy ametajwa kuwania vipengele viwili katika Tuzo za Kimataifa za Zambia ziitwazo Zikomo Awards.
Stevo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na video ya wimbo wake “Fresh Barida”, anawania tuzo hizo kupitia vipengele vya BEST UPCOMING ARTIST OF THE YEAR na BEST SONG OF THE YEAR.
Kumpigia kura Stevo The Simple Boy ni rahisi, ingia kwenye tovuti ya tuzo hizo http://www.zikomoawards.com kisha nenda kwenye category iliyoandikwa Music & Film, baada ya hapo unamu-nominate.