Entertainment

Suge Knight Amshauri Diddy Kufika Mahakamani na Kusema Ukweli Wake

Suge Knight Amshauri Diddy Kufika Mahakamani na Kusema Ukweli Wake

Rais wa zamani wa Death Row Records, Suge Knight, ambaye amekuwa mpinzani wa muda mrefu wa msanii na mfanyabiashara Sean “Diddy” Combs, amemtaka mwanamuziki huyo maarufu kufika kizimbani na kueleza ukweli wake katika kesi inayomkabili, akiamini kuwa hatua hiyo inaweza kuushawishi vizuri upande wa majaji.

Katika mahojiano ya simu na Laura Coates wa CNN, Knight alisisitiza umuhimu wa Combs kujionyesha kama binadamu wa kawaida.
 “Ninaamini kama atasimama na kusema ukweli wake, basi atapata nafasi ya kuachiwa,” Knight alisema. “Kama Puffy atasema, ‘Nilikua natumia madawa ya kulevya. Sikuwa na udhibiti wa maisha yangu au nafsi yangu,’ basi ataweza kujihumanisha, na jopo la majaji linaweza kumuelewa.”
Knight, ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 28 jela kwa kosa la kuua mtu kwa makusudi kupitia ajali ya gari mwaka 2015, alionya kuwa ukimya unaweza kuathiri kesi ya Combs.
“Kama ataendelea kukaa kimya, itaonekana kama anaogopa ukweli. Anatakiwa kuwa na imani na Mungu, avae suruali zake, asimame na aseme ukweli wake,” alisema Knight.
Sean “Diddy” Combs amekana mashtaka ya kupanga njama ya uhalifu (racketeering), usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, na usafirishaji kwa nia ya ukahaba. Ikiwa atapatikana na hatia kwa mashtaka yote, anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *