
Lebo ya Swangz Avenue imethibitisha kumfuta kazi meneja wa msanii wao Vinka kwa madai ya kufuja pesa za booking.
Katika taarifa iliyotolewa na Swangz Avenue, meneja huyo aitwaye Navit Miles hafanyi kazi tena na Lebo hiyo huku ikionya umma kutoshirikiana na Navit kwenye biashara yeyote inayohusiana na Swangz Avenue.
Chanzo cha karibu na lebo hiyo kimefichua kuwa jamaa huyo alitimuliwa kazi kwa ubadhirifu wa pesa za msanii wake Vinka ikizingatiwa kuwa yeye ndiye alikuwa anaratibu shows za msanii huyo.
“Ni kuhusu fedha. Mabosi wake hawakufurahishwa na jinsi alivyoshughulikia malipo aliyopewa na mteja kwa ajili ya kupata huduma za Vinka. Hakuwasilisha pesa zote kwa kampuni hiyo,” chanzo kilifichua.
Swangz Avenue ni lebo kubwa zaidi nchini Uganda na kwa sasa ina wasanii wanne waliosainiwa katika lebo hiyo, Winnie Nwagi, Vinka, Azawi na Zafarani.Wasanii hao kila mmoja ana timu ambayo inajumuisha meneja na wasaidizi.