THE GAME NA TIMU YAKE WAKASIRIKA, WAHOJI NI KWANINI DR. DRE ALIMCHAGUA 50 CENT KWENYE SUPER BOWL 2022

THE GAME NA TIMU YAKE WAKASIRIKA, WAHOJI NI KWANINI DR. DRE ALIMCHAGUA 50 CENT KWENYE SUPER BOWL 2022

Stori kubwa wiki hii kwenye burudani ni Super Bowl Half Time Show ambayo inatajwa kuwa ya kihistoria, lakini The Game ana malalamiko yake. Baada ya 50 Cent kupandishwa na kutumbuiza kama Guest Artist, Rapa The Game pamoja na timu yake wameonekana kutopenda uamuzi huo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, The Game ame-share ujumbe uliowekwa na miongoni mwa memba kwenye timu yake, ambao unasema inakuaje wanampa 50 Cent hiyo nafasi na sio The Game? Game alistahili kuwepo kwenye Jukwaa hilo pia Kauli ya The Game imekuja mara baada ya Super Bowl 2022 Halftime Show kufunguliwa kwa perfomance ya Dr. Dre na Snoop Dogg kupitia ngoma ya “The Next Episode” na “California Love” ya Tupac Shakur, ambapo Rapa na mfanyabiashara 50 Cent alitokea kwenye dakika ya 3:10 kupiga performance ya kufa mtu na ngoma ya “In Da Club” na kuamsha shangwe la aina yake. Eminem ndiye alimpa mashavu 50 Cent kutumbuiza kwenye halftime ya Super Bowl 2022. Eminem ndiye alitoa wazo hilo na kupitishwa na Dre pamoja na wote ambao walikuwa kwenye orodha ya watumbuizaji rasmi. Ikumbukwe Mtayarishaji mkongwe  kutoka Marekani Dr. Dre alitumia shillingi millioni 795 za Kenya kwa ajili ya kutayarisha performance nzima ya Halftime kwenye fainali za Super Bowl 2022 zilizofanyika Februari 14 katika uga wa SoFi huko California. Dunia ilishuhudia Dr. Dre akiandika historia akiwa na wakali wa Hip Hop nchini Marekani; kama Kendrick Lamar, Snoop Dogg, Eminem, 50 Cent na mwanadada Mary J Bridge.

Read More
 50 CENT KUJA NA FILAMU ITAKAYOANGAZIA MAUJI YA MARAPA NCHINI MAREKANI

50 CENT KUJA NA FILAMU ITAKAYOANGAZIA MAUJI YA MARAPA NCHINI MAREKANI

Nyota wa muziki wa kutoka Marekani 50 Cent ambaye kwa sasa amejikita zaidi kwenye uandaaji wa Filamu na uigizaji ametangaza kuachia tamthia itakayoonesha Kesi za mauaji ya Rapa mbalimbali ambazo zimeshindwa kupatiwa ufumbuzi. 50 anaandaa tamthilia hiyo kwa kushirikiana na Mona Scott-Young Monami na Lionsgate. Tamthilia hiyo itaongozwa na Van Lathan ambaye ni mshindi wa tuzo ya Oscar kupitia kipengele cha muongozaji bora wa Filamu fupi ya Two Distant Strangers. Tamthia hiyo itaitwa Hiphop Homicides na 50 Cent anataka kuonesha mambo yote maovu ambayo hupelekea mauaji ya wasanii wa HipHop ambayo yanarindima kila siku nchini Marekani.

Read More
 50 CENT ATANGAZA KUSTAAFU MUZIKI MARA BAADA YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

50 CENT ATANGAZA KUSTAAFU MUZIKI MARA BAADA YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Nguli wa muziki wa hiphop kutoka nchini Marekani 50 Cent  ametangaza kuacha muziki mara baada tu atakapoachia album yake mpya ambayo ana mpango wa kuiachia hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa instagram rapa huyo ambaye amekuwa game ya muziki wa Hiphop kwa miaka 14 amesema amekuwa kwenye game ya muziki kwa muda mrefu na sasa ni wakati wake wa kupumzika na kuacha wasanii wengine waendelee.  “Smile my next album might be the my last terrorized hiphop for 14 years”ameandika 50 Cent kwenye Instagram yake. Taarifa 50 Cent kustaafu muziki imewaacha mashabiki zake na mshangao kwani wengi wamekuwa na kiu ya muziki wake baada ya kuachia album yake ya  Animal Ambition ya mwaka wa 2014. Ikumbukwe wasanii wengi nchini marekani wamekuwa wakitangaza kuacha muziki lakini mwisho wa siku wanarejea tena kwenye muziki ingawa baadhi ya mashabiki wa muziki duniani wanahisi huenda keysha cole tayari amefanya ya kustaafu muziki.

Read More
 50 CENTS ATANGAZA KUJA NA SERIES MPYA “QUEEN NZINGA”

50 CENTS ATANGAZA KUJA NA SERIES MPYA “QUEEN NZINGA”

Mkongwe wa muziki wa Hiphop kutoka Marekani 50 Cent ameuweka muziki kando, anaendelea kujikita kwenye upande wa kutayarisha filamu na vipindi vya televisheni. Siku chache baada ya kutangaza kuja na series ‘Murder Was the Case’ ambayo itagusia historia ya kweli ya rapa Snoop Dogg, 50 Cent ametangaza tena ujio wa series mpya nyingine chini ya Starz. Kupitia ukurasa wake wa instagram, 50 Cent alitudokeza kuhusu ujio wa series iitwayo ‘Queen Nzinga’ ambayo itaangazia na kujikita kwenye maisha ya malkia huyo wa Kiafrika katika Karne 17 nchini Angola. Uhusika mkuu utavaliwa na Yetide Badaki ambaye pia ni mtayarishaji mkuu series hiyo.

Read More
 50 CENT KUILETA “MURDER WAS THE CASE” KWENYE RUNINGA YAKO AKISHIRIKIANA NA SNOOP DOGG

50 CENT KUILETA “MURDER WAS THE CASE” KWENYE RUNINGA YAKO AKISHIRIKIANA NA SNOOP DOGG

Mwaka 1993 wakati Snoop Dogg akirekodi album yake ‘Doggystyle’ alikumbana na kesi ya mauaji kufuatia Kifo cha member wa kundi hasimu ambapo ilidaiwa aliuawa kwa kupigwa risasi na bodyguard wa Snoop Dogg. Album hiyo ya Snoop Dogg ilienda sambamba na usikilizwaji wa kesi yake kiasi cha kupelekea mauzo ya album hiyo kupaa juu na kutengeneza historia kufuatia pia wimbo ‘Murder Was the Case’ uliokuwemo kwenye album hiyo. 50 Cent akiwa kama mtayarishaji mkuu ametangaza ujio wa series iitwayo ‘Murder Was the Case’ chini ya STARZ akishirikiana na rapa Snoop Dogg ambapo itaangazia kisa chote cha tukio hilo ambalo lilimuweka Snoop chini ya ulinzi hadi February 20, 1996 alipoachiwa huru.

Read More