ALI KIBA ADOKEZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA MWAKA WA 2022

ALI KIBA ADOKEZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA MWAKA WA 2022

Hitmaker wa ngoma ya Utu’ msanii Ali Kiba amegusia uwezekano wa kuachia album yake nyingine ifikapo mwakani 2022. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Msanii huyo wa Bongofleva amesema anafikiria kuachia album nyingine mwaka ujao hii ni baada ya album yake mpya Only One King aliyoiachia mwaka huu kufanya vizur kupitia digital platforms mbali mbali. “Thinking of releasing another album 2022!!!”..ameandika Ali Kiba kupitia ukurasa wake wa Twitter. Mpaka sasa Ali Kiba ameshaingiza sokoni album tatu na endapo ataachia album mpya mwaka 2022 itakuwa ni album ya nne tangu aanze safari yake ya muziki

Read More
 ONLY ONE KING ALBUM YA ALI KIBA NDANI YA TIMES SQUARE,NEW YORK.

ONLY ONE KING ALBUM YA ALI KIBA NDANI YA TIMES SQUARE,NEW YORK.

Album mpya ya msanii Ali kiba “Only One King” inazidi kuweka historia mara baada ya cover la album hiyo kuonekana katika Screen za eneo maarufu Times Square huko Jijini New York, nchini Marekani. Album hiyo ambayo ina siku tatu tangu iachiwe, ina kuwa kazi ya kwanza Kwa Ali kiba kuonekana Times Square sehemu ambayo matangazo makubwa duniani huonekana. Sanjari na hilo “Only One King” album imefanikiwa kufikisha jumla ya Streams Milioni 1 katika mtandao wa BoomPlay tangu iachiwe rasmi Oktoba 7. Album hiyo ambaye ni ya tatu kwa mtu mzima Ali Kiba ina nyimbo 16 alizoshirikisha wasanii kutoka Tanzania, Kenya na Nigeria. Miongoni mwa nyimbo zilizoko ni Utu, Let me, Niteke, Bwana mdogo, Happy, na nyingine nyingi.

Read More