Amber Ray Asema Uhusiano Wake na Rapudo Ulivunjika kisa Chai
Sociliate kutoka Kenya, Amber Ray, ameibua gumzo mtandaoni baada ya kufunguka chanzo cha kuvunjika kwa uhusiano wake na mchumba wake, Kennedy Rapudo. Akizungumza kwenye mahojiano na Obinna TV, Amber amesema uhusiano wao uliingia doa baada ya Rapudo kumlazimisha kupika chai wakati yeye alikuwa na hangover kali. Amesema ingawa huwa mnyenyekevu kwa baba wa mtoto wake, alikasirishwa na kitendo hicho kwa sababu hapendi kufanya jambo lolote kwa kulazimishwa. Mama huyo wa mtoto mmoja, amesema baada ya kisa hicho, walikaa bila kuwasiliana kwa takriban mwezi mmoja kabla ya Rapudo kumtafuta ili kusuluhisha tofauti zao. Hata hivyo, amekiri kuwa hadi sasa wameachana mara tatu na kurudiana, akionyesha kuwa uhusiano wao umekuwa na changamoto kadhaa lakini pia maelewano.
Read More