Nadia Mukami afunguka kutengana na Arrow Boy

Nadia Mukami afunguka kutengana na Arrow Boy

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami amefunguka kuhusu madai ya kutengana na baba ya mtoto wake Arrow Bwoy. Katika mahojiano na Mungai Eve, Nadia amesema kuwa alitengana na Arrow Bwoy baada ya kulemewa na mambo mengi ambayo yalitokea katika maisha yake katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. “Imekuwa moja ya miaka mbaya zaidi kwangu. Mungu amenibariki na pia nimepitia changamoto kwa viwango sawa. Nimepitia mengi, mambo yanaweza kuwa makubwa na inaweza kufikia mahali ukavunjika,” alisema. Aidha amewasuta watu ambao walidai alikuwa akifanya kiki kwa ajili ya kutangaza biashara yake mpya ya urembo iliyofunguliwa jijini Nairobi mapema wiki hii. “Haiwezi kuwa mbinu ya kutangaza biashara. Iliikuwa ni sadfa tu. Watu wanaoweza kunielewa wanajua kwamba nimeolewa hivi majuzi, nimepata mtoto na inaweza kulemea mtu, utapanga virago, ni mambo mengi,” alisema Msanii huyo mwenye umri wa miaka 26 amesema licha ya kutengana na baba ya motto wake bado wanasaidia majukumu ya kuwalea motto wao, Haseeb Kai ikizingatiwa kuwa bado wanaisha katika nyumba moja. Lakini pia amezungumzia ishu ya Eric Omondi kumkosoa kwa kushindwa kuwekeza kwenye suala la branding katika mitandao ya kijamii kwa kusema kuwa amejifunza kitu kwenye kauli ya Omondi na atalifanyia kazi suala hilo. Kauli ya Nadia Mukami imekuja mara baada ya kuzindua biashara yake iitwayo ‘Nadia’s Nailbar & Beauty Parlor’ ambayo itahusika na masuala yote ya urembo. Akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa Nadia’s Nailbar & Beauty Parlor’, nadia alisema uzinduzi wa biashara yake hiyo ni moja kati ya ndoto ambazo amekuwa akitamani kufanikisha katika maisha.

Read More
 Nadia Mukami athibitisha kuachana na Arrow Boy

Nadia Mukami athibitisha kuachana na Arrow Boy

Staaa wa muziki nchini Nadia Mukami amethibitisha kutengana na mwanamuziki mwenzake Arrow Bwoy. Katika taarifa ambayo aliichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nadia alibainisha kuwa yeye na mzazi huyo mwenzake hawajakuwa pamoja kwa muda mrefu sasa. aidha alikiri kuwa ameshindwa kabisa kuendelea kudanganya kuhusu uhusiano wao kwa watu wengi ambao hawakuwa na ufahamu kuhusu kutengana kwao. “Ili tu kuwafafanulia watu wanaojaribu kubook mimi na Arrow Bwoy, nimeishiwa na uwongo. Hatujakuwa pamoja kwa muda, tuliachana,” Nadia Mukami aliandika kwenye Instastory yake leo Alhamisi. Hata hivyo Nadia amesisitiza kuwa ni kweli ameachana na Arrow Boy na hatumii suala hilo kutafuta kiki kama wengi wanavyodhani kwa kuwa tayari ana jina kubwa kwenye muziki nchini Kenya. Nadia Mukami na Arrow Boy wamekuwa wapenzi kwa muda sasa na kwa pamoja wamebarikiwa kumpat motto mmoja aitwaye Haseeb Kai.

Read More
 Nadia Mukami afunguka juu ya mpango wa kupata mtoto wa pili

Nadia Mukami afunguka juu ya mpango wa kupata mtoto wa pili

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Nadia Mukami amefichua kuwa hana mpango wa kupata mtoto mwingine hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram akimjibu shabiki aliyetaka kujua ni lini atampata mtoto wake wa pili, Nadia amesema kwa sasa hajajiandaa kisaikolojia kupata uja uzito mwingine huku akisisitiza kuwa atafanya hivyo labda miaka mitano ijayo. “Labda baada ya miaka mitano, sitaki saa hii! Eh ni kujitolea pakubwa sana,” Mukami alisema. Nadia kwa sasa ni mama ya mtoto mmoja aitwaye Kai aliyepata na mchumba wake Arrow Boy miezi minane iliyopita.

Read More
 NADIA MUKAMI ADOKEZA UJIO WA EP YA PAMOJA NA ARROW BWOY

NADIA MUKAMI ADOKEZA UJIO WA EP YA PAMOJA NA ARROW BWOY

Mwanamuziki Nadia Mukami amedokeza kuja na EP ya pamoja na mchumba wake Arrow Boy kwa sababu wamekuwa na muendelezo mzuri wakuachia nyimbo kali.   Kwenye mahojiano hivi karibuni Nadia amesema wana nyimbo nyingi ambazo hazijatoka ambapo amewataka mashabiki wakae mkao wa kula kupokea EP yao ya pamoja ambayo ameitaja kuwa moto wa kuotea mbali.   Katika hatua nyingine ametupasha kuhusu maendeleo ya album yake mpya kwa kusema kwamba album yake hiyo ipo kwenye hatua za mwisho kukamilika na itakuwa ya kitofauti sana kwani itaangazia safari yake ya maisha kabla na baada ya umaarufu.   Hitmaker huyo “Maombi” amesema album hiyo ilipaswa kutoka mapema mwaka huu lakini kutokana na yeye kushikika na majukumu ya malezi aliamua kuachia EP iitwayo Bundle of Joy ambayo ilikuwa mahsusi kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya mtoto.

Read More
 ARROW BOY AWAPA SOMO VIJANA WA KIUME KUHUSU MPANGO WA UZAZI

ARROW BOY AWAPA SOMO VIJANA WA KIUME KUHUSU MPANGO WA UZAZI

Hitmaker wa “Enjoy”, Msanii Arrow Boy ametoa changamoto kwa vijana wa kiume kujipanga kimawazo na kifedha kabla ya kuwapa wapenzi wao uja uzito. Kupitia kurasa zake za mitadao ya kijamii, Arrow Boy amesema safari ya uja uzito inakuja na changamoto nyingi, hivyo ni vyema kwa kijana wa kiume kutumia kinga kama hayuko tayari kubeba mzigo wa uzazi. Bosi huyo wa Utembe World ameenda mbali Zaidi na kuhoji kuwa ikitokea kijana wa kiume amempa binti wa watu uja uzito bila kutarajia anapaswa kutoa ushirikiano kwenye suala la kutoa matunzo kwa mama pamoja na mtoto. “Boychild kama hauko ready na hizi mbwe mbwe za pregnancy journey tumia tu jwala na ukijipata hapa please cooperate #Kaiwangu trending on YouTube”. Ameandika Arrow Boy. Utakumbuka kipindi Nadia Mukami alikuwa mja mzito, Arrow boy alikiri hadharani kupitia changamoto kibao kwenye safari yake ya uja uzito lakini mwisho wa siku alifanikiwa kumliwaza baby mama wake huyo kwa kumpa mahitaji ya msingi.

Read More
 ARROW BOY AFUNGUKA ISHU YA KUBADILI DINI YA MPENZI WAKE NADIA MUKAMI

ARROW BOY AFUNGUKA ISHU YA KUBADILI DINI YA MPENZI WAKE NADIA MUKAMI

Staa wa muziki nchini Arrow Boy amefunguka ishu ya mpenzi wake nadia mukami kubadilisha dini kutoka ukristo kwenda uislamu. Katika mahojiano yake hivi karibuni baada ya kuwasili kutoka nchini Ethiopia ambako alienda kwa ajili ya show yake, Arrow Boy amesema hana mpango kumfanya Nadia Mukami abadilishe dini hasa wakati wanaelekea kufunga ndoa yao kwa kuwa upendo ndio kitu kilichowaleta pamoja. Mbali na hayo Arrow Boy kwa mara ya kwanza amekiri hadharani kutokuwa mwanachama wa chama cha muziki na hakimiliki nchini MCK huku akitoa changamoto kwa wasanii wa kenya kuacha kuifanya bodi ya PRISK mzaha mtandaoni na badala yake waungane kwa ajili ya kuleta mabadilliko kwenye bodi zilizopewa jukumu za kusimamia mirabaha ya wasanii. Utakumbuka Arrow boy ambaye vizuri na album yake ya Focus kwa sasa anajianda kuanza tour yake ya muziki barani ulaya hivi karibuni.

Read More
 ARROW BOY AVUNJA KIMYA CHAKE BAADA YA OTILE BROWN KUIPONDA ALBUM YAKE YA FOCUS

ARROW BOY AVUNJA KIMYA CHAKE BAADA YA OTILE BROWN KUIPONDA ALBUM YAKE YA FOCUS

Nyota wa muziki nchini Arrow Bwoy amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya Otile Brown kudai kuwa hakufurahishwa na kitendo chake cha kushirikisha wimbo wao ambao haukuwa umekamilika kwenye album yake mpya. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio, Arrow Bwoy amesema yuko tayari kusuluhisha tatizo lililopo kati yake na Otile Brown huku akidai hakuwa na ufahamu kuhusu kutoridhika kwa Otile Brown kwa sababu alijieleza kupitia mitandao ya kijamii na yeye hamfuatilii. Kulingana na Arrow boy, malumbano hayatamfaidi yeye wala Otile Brown, hivyo usimamizi wake utawasiliana na bosi huyo wa Just In Love ili kutafuta suluhu. Kauli ya Arrow Boy imekuja baada ya Otile Brown kumsuta vikali kwa hatua yake ya kukwenda kinyume na mkataba wa makubaliano wa kutoachia demo ya wimbo wao wa pamoja huku akisema kwamba kitendo hicho huenda ikamshushia brand yake ya muziki ambapo alienda mbali Zaidi na kumtaka Arrow Boy aundoe wimbo wao kwenye digital platfoms mbali mbali kabla hajachukua hatua kali za kisheria. Utakumbuka Arrow Boy alimshirikisha Otile Brown kwenye wimbo uitwao Show me ambao unapatikana kwenye Albamu yake mpya iitwayo Focus ambayo ina jumla ya ngoma 14 za moto.

Read More
 ARROW BOY AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA “FOCUS”

ARROW BOY AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA “FOCUS”

Staa wa muziki nchini Arrow Boy ameachia rasmi album yake mpya iitwayo ” Focus ” ambayo ina jumla ya ngoma 14 za moto. Album hiyo ambayo kwa sasa inapatikana kupitia majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani, ina kolaba 7 kutoka kwa wakali kama Spice Diana, Otile Brown, B Classic, Nadia Mukami,Sanaipei Tande, Nandy na Dufla Diligion. Focus album ina nyimbo kama Show Me, Mood, Enjoy, Raha,Uko Nami,Usinimwage,Fall, Njiwa na nyingine kibao. Focus album ni album ya pili kwa mtu mzima Arrow Boy baada ya Hatua iliyotoka mwaka wa 2019.

Read More
 NADIA MUKAMI AVISHWA PETE YA UCHUMBA NA ARROW BOY

NADIA MUKAMI AVISHWA PETE YA UCHUMBA NA ARROW BOY

Msanii nyota nchini Arrow Boy amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake Nadia Mukami ambaye pia ni mwanamuziki. Kwenye performance yao  katika hafla ya uzinduzi wa Focus album Usiku wa kuamkia Machi 13 jijini Nairobi, Arrow Boy alipiga goti na kumvisha Pete Nadia Mukami ambapo alienda mbali zaidi na kuahidi yupo tayari kufunga nae ndoa,  jambo lilomfanya Nadia Mukami amwage machozi ya furaha huku mashabiki wakiwashangilia kwa hatua ya kuanika wazi mahusiano yao. Haya yanajiri ikiwa ni  siku chache baada ya Wawili hao kuweka wazi kuwa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza kwenye uzinduzi wa wakfu wao wa “Lola & Safari” Utakumbuka Mwezi Agosti mwaka wa 2021 Nadia Mukami pamoja na Arrow Boy walithibitisha kuwa wapenzi mara baada ya kuwa kwenye mahusiano ya siri kwa muda mrefu.

Read More
 ARROW BOY AKANUSHA MADAI YA KUTUMIA KIKI KUTANGAZA MUZIKI WAKE

ARROW BOY AKANUSHA MADAI YA KUTUMIA KIKI KUTANGAZA MUZIKI WAKE

Msanii nyota nchini Arrow Boy, amesema yeye haitaji kiki ili kazi zake ziweze kufanya vizuri sokoni, tofauti na wasanii wengi wa sasa hivi. Akiwa Instagram Live Arrow Boy amesema kazi nzuri inajitangaza yenyewe bila kiki, kwani msanii anaweza tengeneza kiki kubwa alafu kazi yake ikawa haina ubora, na kushusha hadhi ya muziki wake. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Unconditional Love” amesema kuwa wasanii wengi wamejikita kwenye kutafuta kiki badala ya kuwapa mashabiki ladha tofauti na kusisitiza kwamba dhana ya kiki inapaswa kufutika ili kila mtu afanye kazi nzuri. Hata hivyo amewataka wasanii wenzake waache kutafuta ‘kiki’ ili kupata majina makubwa kwenye muziki bali wajikite kwenye kutengeza kazi nzuri. Kauli ya Arrow Boy imekuja mara baada ya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kutilia ziara yake ya “Meet The People Tour” kwenye baadhi ya mitaa jijini Nairobi ambapo alipata fursa ya kula chakula na kupiga stori mashabiki zake lakini pia aliwalipia nauli, kitu ambacho kiliwafanya walimwengu kuhoji kuwa alikuwa anatumia jambo hilo kutafuta kiki kwa ajili ya kuitangaza album yake mpya iitwayo Focus itakayoingia sokoni Machi 12 mwaka wa 2022.

Read More
 ARROW BOY ATANGAZA RASMI MAHALA PATAKAPO FANYIKA UZINDUZI WA ALBUM YAKE MPYA

ARROW BOY ATANGAZA RASMI MAHALA PATAKAPO FANYIKA UZINDUZI WA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa muziki nchini Arrow Boy ametangaza rasmi mahala patakapo fanyika uzinduzi wa Album yake mpya iitwayo ‘Focus’. Kupitia ukurasa wake wa instagram mkali huyo wa ngoma ya Unconditional ametujuza kuwa Album hiyo ambayo itaachiwa rasmi tarehe 12 mwezi huu, uzinduzi wake utafanyika Katika ukumbi wa ‘The Junction Mall’ uliopo , Jijini Nairobi. Bosi huyo wa lebo ya muziki ya Utembe World amewataka mashibiki ku-pre-order tiketi za kuhudhuri uzinduzi wa album yake ya Focus kupitia wavuti mtickects.com huku akiwataja  Nadia Mukami, Sanaipei Tande, Iyaani, Kristoff, Hart The Band, na Dufla Diligon kama baadhi ya wasanii watakaomsindikiza kwenye uzinduzi wa album yake hiyo. Licha ya kuweka wazi jina na cover ya album yake mpya, Arrow Boy hajatuambia idadi ya ngoma na wasanii aliowashirikisha kwenye album yake ya Focus. Focus album inaenda kuwa album ya pili kwa mtu mzima Arrow Boy baada ya Hatua iliyotoka mwaka wa 2019.

Read More
 NADIA MUKAMI ANYOSHA MAELEZO KUHUSU TETESI ZA KUACHANA NA MPENZI WAKE ARROW BOY

NADIA MUKAMI ANYOSHA MAELEZO KUHUSU TETESI ZA KUACHANA NA MPENZI WAKE ARROW BOY

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami amekanusha madai ya kumu unfollow mchumba wake Arrow Boy kwenye mtandao wa Instagram. Akijibu shabiki yake kwenye mtandao wa instagram aliyetaka kujua hali ya uhusiano wake kwa sasa na Arrow Boy, Nadia Mukami amesema hajawahi fuatilia na Arrow Boy kwenye mtandao huo huku akithibitisha kuwa uhusiano wake na hitmaker huyo wa ngoma ya Unconditional Love upo imara licha ya uvumi unaosambaa mitandaoni kuwa hawana maelewano mazuri. Nadia Mukami ameyaweka hayo wazi wakati akitangaza ujio wa album mpya  ya Arrow boy iitwayo Focus inayotarajiwa kuingia sokoni machi 12 mwaka wa 2022. Mapema wiki hii mitandao nyingi ya udaku nchini iliripoti kuwa uhusiano wa Nadia Mukami na Arrow Boy umeingia na ukungu mara baada ya wasanii hao kutoonekana wakifuatilia kwenye mtandao wa Instagram. Utakumbuka Mwezi agosti mwaka wa 2021 Nadia Mukami na Arrow Boy walithibitisha kuwa wapenzi mara baada ya kuwa kwenye mahusiano ya siri kwa muda mrefu. Hitmaker huyo wa Maombi alienda mbali na kueleza kuwa aliahamua kuyaweka wazi mahusiano yake na Arrow Boy kwa sababu tayari alikuwa amekuwa kiakili kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Read More