ARROW BOY KUACHIA ALBUM YAKE MPYA MWEZI MACHI MWAKA HUU

ARROW BOY KUACHIA ALBUM YAKE MPYA MWEZI MACHI MWAKA HUU

Mwanamuziki nyota nchini Arrow Boy ameachia rasmi Cover ya album yake mpya iinayokwenda kwa jina la “Focus” Kupitia ukurasa wake instagram Arrow Boy ametuonyesha cover ya album yake mpya huku akiwataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kuipokea Album hiyo ambayo itaingia sokoni machi 12 mwaka wa 2022. Licha ya kuweka wazi jina na cover ya album yake mpya, Arrow Boy hajatuambia idadi ya ngoma na wasanii aliowashirikisha kwenye album yake ya Focus. Focus album inaenda kuwa album ya pili kwa mtu mzima Arrow Boy baada ya Hatua iliyotoka mwaka wa 2019.

Read More
 NADIA MUKAMI AFUNGUKA MAZITO KUHUSU UJA UZITO WAKE NA ARROW BOY

NADIA MUKAMI AFUNGUKA MAZITO KUHUSU UJA UZITO WAKE NA ARROW BOY

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami ameshindwa kuvumilia kinachoendelea mtandaoni kuhusu uja uzito wake na Arrow boy. Kupitia video aliyoishare kwenye ukurasa wake wa instagram Nadia Mukami amedokeza kuwa alipoteza uja uzito wake mwishoni mwa mwaka wa 2021. Hitmaker huyo wa “Roho Mbaya” amesema licha ya kupoteza uja uzito wake aliahuma kutoweka wazi habari hiyo mbaya kwa umma. Hata hivyo amemtolea uvivu Jalang’o kwa  madai ya kusema kuwa hataomba msamaha kwa hatua ya kuanika uja uzito wake akiwa redioni akisema kwamba kitendo hicho sio cha kingwana.. Kauli ya Nadia Mukami imekuja mara baada ya Jalang’o kutangaza redio kuwa anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza na mchumba wake Arrow Boy hivi karibuni. Jambo ambalo lilimkasirisha Arrow Boy ambapo alitumia instastory kumuonya Jalang’o akome kuingilia maisha yake na nadia mukami. Kutokana na hilo Jalang’o alimjibu Arrow Boy kwa kusema kwamba atakoma kuzungumzia maisha yao na hajutii kuweka wazi uja uzito wa Nadia Mukami.

Read More
 ARROW BOY AMVUA NGUO JALANG’O, AMTAKA AACHE KUFUATILIA MAISHA YAKE NA NADIA MUKAMI

ARROW BOY AMVUA NGUO JALANG’O, AMTAKA AACHE KUFUATILIA MAISHA YAKE NA NADIA MUKAMI

Staa wa muziki nchini Arrow Boy kwa mara nyingine amekanusha tetesi za mchumba wake Nadia Mukami kuwa na uja uzito wake. Hii ni baada ya mchekeshaji Jalang’o kwenye kipindi cha Jalas and Kamene in the morning kinachoruka kupitia Kiss 100 kusisitiza kuwa Nadia Mukami ni mjamzito na alithibitisha hilo wakati wapenzi wawili hao walimtembelea kijiji kwao. Jalango alienda mbali zaidi na kumshauri Nadia Mukami aache ishu ya kuficha uja uzito kwa umma kwani hivi karibuni itajulikana tu. Sasa akijibu hilo Arrow Boy kupitia instastory ameandika ujumbe unaosomeka “2022 Wanaume Tupunguze Mshene Bana biashara Haikuhusu achana nayo Kabisa shugulika na maisha yako” ujumbe ambao umetafsiri kumlenga moja kwa moja Jalang’o. Juzi kati Nadia Mukami aliripotiwa kuwa na uja uzito wa Arrow Boy hii ni baada ya kuonekana akitumbuiza kwenye show moja akiwa amevalia mavazi makubwa jambo ambalo liliwafanya wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa hitmaker huyo wa “Roho Mbaya” ni mjamzito. Hata hivyo Nadia Mukami kupitia Instagram page yake amenyosha maelezo kwa kupost picha ambayo imezima kabisa tetesi za kuwa na uja uzito.

Read More
 ARROW BOY AKANUSHA TUHUMA ZA KUWA NA BABY MAMA

ARROW BOY AKANUSHA TUHUMA ZA KUWA NA BABY MAMA

Nyota wa muziki nchini Arrow Boy amekanusha tuhuma za kumtekeleza Baby mama wake. Akijibu swali la shabiki yake aliyetaka kujua kama ana mtoto kwenye kikao cha maswali na majibu kwenye mtandao wa instagram Hitmaker huyo wa usinimwage amesema hana mwanamke yeyote zaidi ya Nadia Mukami. Ikumbukwe mwezi Agosti mwaka huu Arrow Boy alituhumiwa kumtekeleza Baby mama wake ambaye wamedumu kwenye ndoa kwa takriban miaka kumi. Tuhuma hizo ziliibuliwa na mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii kupitia insta story ya mwanablogu mwenye utata Edgar Obare kwenye mtandao wa Instagram.

Read More