Azawi Asaini Mkataba Mpya na Swangz Avenue
Msanii kutoka Uganda, Priscilla Zawedde, anayejulikana kwa jina la kisanii Azawi, ametia saini mkataba mpya na lebo kubwa ya muziki Swangz Avenue kwa mara ya pili. Akizungumza baada ya kusaini, Azawi amesisitiza kuwa ushirikiano wake na Swangz Avenue umekuwa nguzo muhimu katika kukuza kipaji chake. Msanii huyo anasema mkataba huo mpya ni motisha wa kuendeleza ubunifu na kupanua wigo wa kazi zake. Azawi alijiunga na Swangz Avenue mwaka 2019, na tangu wakati huo amepanda ngazi hadi kuwa miongoni mwa nyota wakubwa wa muziki si tu nchini Uganda, bali pia katika ukanda wa Afrika Mashariki. Safari yake ya muziki imekuwa ya mafanikio makubwa, ikianzia na Lofit EP mwaka 2020, ikafuatiwa na albamu ya African Music mwaka 2021, albamu ya Sakofa mwaka 2023, na Lost Files EP iliyotoka mwaka huu.
Read More