Entertainment

Azawi Asema Wasanii Wakongwe Uganda Wanatumia Uchawi

Azawi Asema Wasanii Wakongwe Uganda Wanatumia Uchawi

Msanii nyota kutoka Swangz Avenue, Azawi, amezua gumzo kubwa katika tasnia ya muziki baada ya kudai kuwa baadhi ya wanamuziki wakongwe nchini Uganda wanatumia uchawi na mbinu chafu ili kuwapoteza wasanii wapya wanaochipukia kwenye muziki.

Kupitia mahojiano aliyofanya hivi karibuni, Azawi amesema kuwa muziki nchini humo umekuwa na mazingira magumu kwa vipaji vipya, akidai kuwa kuna wasanii waliotawala tasnia kwa miaka mingi ambao hawawezi kuvumilia ushindani mpya. Kwa mujibu wake, baadhi yao wanatumia vitendo vya kishirikina, uvumi na njama za kuwaharibia sifa ili kuwazuia wasanii wapya kupenya kwenye soko.

Azawi amesema ameona visa mbalimbali vya vijana wenye uwezo mkubwa kukatishwa tamaa au kuondolewa kwenye nafasi muhimu kwa sababu ya hofu na wivu wa wasanii waliotangulia. Hata hivyo ameongeza kuwa badala ya kuwasaidia chipukizi, baadhi ya mastaa hao wamekuwa vizuizi katika ukuaji wa muziki wa Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *