Babu Tale akanusha madai ya Sallam SK kujiunga na Lebo ya Konde Music Worldwide

Babu Tale akanusha madai ya Sallam SK kujiunga na Lebo ya Konde Music Worldwide

Meneja wa Diamond Platnumz na WCB Wasafi kwa ujumla, Babu Tale amesema sio kweli kwamba Sallam SK anajiunga na Lebo ya Harmonize, Konde ‘Gang’ Music Worldwide. Tale amesema amefurahi kuona wawili hao wamemaliza tofauti zao kama ilivyoonekana mitandaoni hivi karibuni lakini sio kweli suala kujiunga na Lebo yake. “Lakini nilipoona juzi wanasalimiana maana yake hakuna shida, ila hii ya kusema Sallam SK kakumbatiana na Harmonize anaenda Konde Gang, eeh, we kuweza!” amesema Babu Tale akiongea na Mjini FM. Itakumbukwa, Sallam anahusishwa zaidi kuwa ndiye atakaye kuwa Meneja wa Harmonize kufuatia video inayowaonesha wawili hao wakisalimiana na kukumbatiana walipokuwa visiwani Zanzibar ambapo Sallam alihudhuria kwenye show ya Harmonize jambo ambalo limeibua hisia chanya kwa mashabiki. Sallam SK ni miongoni mwa Mameneja wa watatu wa Diamond Platnumz na WCB Wasafi, wengine ni Babu Tale na Mkubwa Fella.

Read More
 Babu Tale aburuzwa mahakamani kwa kushinda kulipa fidia ya Ksh millioni 13

Babu Tale aburuzwa mahakamani kwa kushinda kulipa fidia ya Ksh millioni 13

Meneja wa Msanii Diamond Platnumz, Babu Tale ambaye pia mmoja wa wakurugenzi wa kampuni inayojihusisha na shughuli za burudani, Tip Top Connections Company Limited yuko hatarini kufungwa jela kutokana na kushindwa kumlipa mhadhiri wa dini ya Kiislam, Sheikh Hashim Mbonde, fidia ya KSh milioni 13. Tayari Sheikh Mbonde ameshafungua maombi Mahakama Kuu akiiomba mahakama hiyo iamuru BabuTale akamatwe na afungwe kwa kushindwa kumlipa fidia hiyo. Sheikh Mbonde amefungua maombi hayo dhidi ya Tip Top na Babu Tale baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali taarifa yao ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyowaamuru kulipa fidia hiyo, Agosti 17, 2022.

Read More
 ZUCHU KULIPA MILLIONI 500 ZA KENYA KUONDOKA WCB

ZUCHU KULIPA MILLIONI 500 ZA KENYA KUONDOKA WCB

C.E.O wa WCB Wasafi, Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa Zuchu kuondoka katika Lebo hiyo atalipa takriban shilingi milllioni 500 za Kenya. Kauli ya Diamond inakuja muda mfupi baada ya Babu Tale kutangaza Lebo hiyo itasaini wasanii wapya hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Babu Tale ameandika “Hivi karibuni tutasaini wasanii wawili kujiunga lebo ya Wasafi ila safari hii tumeamua msanii atakua na mashaidi wawili kutoka COSOTA na BASATA” “Music ni biashara yetu na ni jukumu letu kukuza na kusimamia hii kazi, hatuwezi kuacha hata iwe vipi” amesema Tale. Hadi sasa WCB iliyoanza kusaini wasanii tangu mwaka 2015, ina wasanii kama Diamond Platnumz, Queen Darleen, Lava Lava, Mbosso na Zuchu. Utakumbuka WCB Wasafi haijasaini msanii mpya tangu Aprili 2020 walipomtangaza Zuchu ambaye alikuwa msanii wa pili wa Kike ndani ya lebo hiyo.

Read More