WAANDAAJI WA BEACH FEST MOMBASA WASUTWA VIKALI KWA KUWAHADA MASHABIKI

WAANDAAJI WA BEACH FEST MOMBASA WASUTWA VIKALI KWA KUWAHADA MASHABIKI

Mashabiki waliohudhuria tamasha la siku tatu laΒ  Beach Fest linaloendelea mjini Mombasa wamegadhabishwa na hatua ya msanii wa Nigeria Omah Lay kukosa kutumbuiza kwenye tamasha hilo usiku wa kuamkia leo. Mashabiki hao wamewasuta vikali waandaaji wa Beach Fest kwa hatua ya kuwaada huku wakikerwa zaidi na suala la maafisa wa polisi kuwafurusha katika eneo la onesho licha ya kulipa shillingi elfu 5 kwa ajili ya kumuona msanii wao pendwa. Hata hivyo wamewataka waandaaji wa Beach Fest kuwaregeshea pesa zao la sivyo watachukulia hatua kali za kisheria kwa madai ya kuwapora fedha zao. Waandaji wa Beach Fest hawajatoa tamko lolote kuhusiana na madai yaliyoibuliwa na baadhi ya mashabiki waliohudhuria tamasha hilo usiku wa kuamkia leo. Ikumbukwe tamasha la Beach Fest linalofanyika katika ukumbi wa burudani wa B-Club mjini Mombasa  lilianza siku ya jana Disemba 31 mwaka 2021 litakamilika Januari  2 mwaka 2022 ambapo wasanii   kama Sauti sol, Marioo, Jovial na wengine wengi wakitarajiwa kutuimbuiza katika tamasha hilo.

Read More