Bensoul afichua sababu za kususia tamasha la Asake Nairobi
Msanii wa muziki kutoka Kenya, Bensoul, ameweka wazi kilichomsukuma yeye na timu yake kususia tamasha la Asake jijini Nairobi, licha ya kuwa shabiki mkubwa wa nyota huyo wa Nigeria. Kwenye mahojiano na Obinna TV, Bensoul amesema walipofika eneo la tamasha kwa ajili ya sound check, walikumbana na hali ya dharau. Anadai kuwa waliamriwa waondoke jukwaani, huku vifaa vyao vikikatiwa umeme katikati ya sound check, jambo alilolitaja kuwa ni dharau ya wazi kwao kama wasanii. Kwa mujibu wa Bensoul, tukio hilo liliwavunja moyo na kuwafanya wachukue uamuzi wa kutopanda jukwaani kabisa, licha ya kuwa tayari ku-perform mbele ya mashabiki wao na wa Asake pia. Kauli ya Bensoul imeibua mjadala mpana mitandaoni, wengi wakikosoa waandaaji wa tamasha kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kukosa mpangilio na kutothamini wasanii wa ndani. Wengine, hata hivyo, wamemsifu Bensoul kwa kusimamia heshima yake na ya wasanii wa Kenya.
Read More