Nay wa Mitego, Billnass na Nandy Wazozana Hadharani

Nay wa Mitego, Billnass na Nandy Wazozana Hadharani

Mzozo mkali wa maneno umeibuka tena kwenye mitandao ya kijamii kati ya wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego, Billnass na mkewe Nandy, ukihusisha tuhuma za fitna, chuki na wivu wa maendeleo. Chanzo cha mvutano huo ni kauli ya Billnass aliyodai kuwa alipitia fitna za kutaka kufungwa kwa kesi ya wizi ambayo Nay wa Mitego alihusishwa nayo kwa kauli zisizo rasmi. Billnass, kupitia mahojiano yake na East Africa Radio, alionesha wazi kutoridhishwa na kile alichokiita hila zilizopangwa dhidi yake na watu aliowahi kuwachukulia marafiki. Baada ya maneno hayo, Nay wa Mitego hakusita kujibu kupitia sehemu ya maoni kwenye posti hiyo. Nay alimtaja Billnass kuwa ni msanii mjinga anayependa kiki bila mipaka na kumuita mwizi ambaye alistahili hata kifungo kwa tabia zake. “Acha nikupe unachotaka, wewe ni mwizi, ungeenda jela kwa tabia yako ya wizi. Nina kazi nyingi za kufanya, siwezi kushughulika na kukukandamiza wewe. Mgande Nandy ivyo ivyo ili usije ukaendelea na udokozi,” aliandika Nay wa Mitego. Kauli hiyo iliwasha moto zaidi pale mke wa Billnass, msanii Nandy, alipoamua kumjibu Nay moja kwa moja kwa hasira kali. Kupitia sehemu ya maoni, Nandy alimshutumu Nay kwa wivu na kumuita mvuta bangi, huku akidai kuwa ana chuki kutokana na kushindwa kimaisha. “Nay wa Mitego wewe cho…k…o, jina langu limeingiaje hapo? Mvuta bangi wewe! Una wivu wa maendeleo. Umejaribu kupambana umeshindwa, umebaki kuwa shabiki. Wa kuibiwa muibiwe nyie, na mnacho cha kuibiwa kwanza? Endelea na chaka zako ujikomboe, maisha upande huu mzito boob utasanda! Kithetheeee wewe, fyuu,” aliandika Nandy kwa hasira. Mashabiki kwenye mitandao wamegawanyika, baadhi wakimtetea Nay kwa kusema anasema ukweli bila uoga, huku wengine wakimtaka apunguze maneno ya matusi na wivu. Wengine wamewaomba wasanii hao warekebishe tofauti zao kwa hekima na busara badala ya kurushiana maneno hadharani. Kwa sasa, hakuna dalili za pande hizi kupoa, na mashabiki wanaendelea kufuatilia kwa karibu kuona ni nani atarushia dongo linalofuata.

Read More
 Upendo wa Nandy kwa Billnass Wagusa Mioyo ya Mashabiki Mitandaoni

Upendo wa Nandy kwa Billnass Wagusa Mioyo ya Mashabiki Mitandaoni

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Nandy, ameonesha kwa mara nyingine ukubwa wa mapenzi yake kwa mume wake ambaye pia ni rapa, Billnass, kwa kauli ya kugusa hisia iliyoacha wengi wakitafakari juu ya upendo wa dhati. Kupitia mahojiano ya hivi karibuni, Nandy alieleza kuwa mapenzi yake kwa Billnass ni ya kipekee kiasi kwamba hawezi hata kufikiria kuendelea kuishi endapo angebaki peke yake. “Nampenda sana Billnass. Ikiwa kuna siku kifo kitatutenganisha, basi ni heri iwe mimi nitaondoka kwanza. Siwezi kuimagine maisha yangu bila yeye,” alisema kwa hisia. Kauli hiyo imezua hisia mseto mtandaoni, wengi wakiguswa na upendo wao wa dhati, huku wengine wakisifia jinsi wawili hao wanavyoendeleza ndoa yao kwa upendo na heshima, licha ya changamoto za maisha ya mastaa. Nandy na Billnass, ambao walifunga ndoa yao rasmi mwaka 2022, wamekuwa mfano wa kuigwa katika jamii, wakionesha mshikamano si tu kwenye maisha ya ndoa bali pia katika kazi zao za muziki. Mara kwa mara wamekuwa wakishirikiana kwenye miradi ya pamoja na kuonesha hadharani mapenzi yao, hali ambayo imewavutia na kuwapa matumaini mashabiki wao. Wakati ambapo ndoa nyingi za mastaa hukumbwa na drama na migogoro, wawili hawa wameendelea kuwa mfano wa kuigwa, huku wakitoa msukumo kwa wengine kuamini katika mapenzi ya kweli.

Read More
 NANDY NA BILLNASS WAPATA MTOTO

NANDY NA BILLNASS WAPATA MTOTO

Msanii wa Bongofleva, Nandy na mume wake, Billnass wamejaliwa kupata mtoto wao wa kwanza. Akithibitisha taarifa hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram Dr Cheni ambaye alikuwa MC wa harusi yao, amewapongeza wawili hao na kuwatakia afya njema pamoja na mtoto wao. “Wow Congratulations Mr and Mrs Billnass na Nandy kwa kupata mtoto Mungu awakizie awalindie kitoto Chenu. Mbarikiwe sanaa” ameandika Dr Cheni. Utakumbuka hivi karibuni Nandy alitangaza kusimamisha tamasha lake, Nandy Festival baada ya kupita kwenye mikoa miwili kati ya mitano nchini Tanzania iliyokuwepo kwenye ratiba yake

Read More
 NANDY AFUNGUKA JUU YA UJAZITO WAKE

NANDY AFUNGUKA JUU YA UJAZITO WAKE

Mwanamuziki wa Bongofleva Nandy  kwa mara ya kwanza ameweza kufunguka machache kuhusiana na ujauzito wake. Akizungumza kwenye sherehe ya ‘kitchen party’ yake wikiendi hii iliyopita Nandy amesema, mumewe mtarajiwa (Billnass) ndio wa kwanza kugundua kuwa  ana ujauzito mara baada ya kuona mabadiliko mbalimbali kama ya kitabia. Lakini pia amebainisha kitu alichokuwa akikitamani ni kupata mtoto akiwa tayari yupo ndani ya ndoa, hivyo kwa namna ilivyotokea amesema ni baraka pia. “Nilikuwa natamani kupata mtoto nikiwa tayari nipo ndani ya ndoa. Nimejaliwa nikiwa bado sijaingia kwenye ndoa lakini huyu mtoto ntaingia nae kwenye harusi na kwenye ndoa hivyo sio kitu kibaya ni baraka na wazazi wote wameridhia” – ameeleza Nandy. Ikumbukwe, Nandy na Billnass ambao kwa sasa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza hivi karibuni, wana mpango kufungua ndoa mwezi huu wa Julai.

Read More
 NANDY NA BILLNASS MBIONI KUPATA MTOTO WAO WA KWANZA.

NANDY NA BILLNASS MBIONI KUPATA MTOTO WAO WA KWANZA.

Mastaa wawili wa muziki kutoka nchini Tanzania Bill Nass na Nandy ambao wamekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi tangu mwaka 2016 wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza pamoja. Nandy kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha hilo kwa kupost picha ya ujauzito wake na kusindikiza na caption inayosomeka “Asante Mungu kwa zawadi hii” Taarifa za Nandy kuwa na ujauzito zilikuwa za muda mrefu lakini bado hazikudhibitishwa na yeye mwenyewe tofauti na ilivyokuwa inadaiwa. Wawili hao wanatarajia kufunga ndoa mwezi huu wa saba baada ya Billnass kumvisha pete ya Uchumba Nandy siku ya Februari 20 mwaka huu

Read More